0

Kutoitambua Israel ndio msingi mkuu wa siasa za Iran 
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kutoutambua utawala wa Kizayuni wa Israel ni katika misingi thabiti na isiyobadilika ya siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu.

Sadeq Hossein Jaberi Ansari amesema hayo leo m
bele ya waandishi wa habari hapa mjini Tehran; na amma kuhusiana na baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni amesema, msimamo thabiti na usioyumba wa Iran tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kutoutambua wala kuupa uhalali utawala wa Kizayuni na kwamba

msimamo huo usiobadilika katika siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu bado uko vile vile.
Jaberi Ansari ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni utawala pandikizi na umeundwa ili kulipora taifa la Palestina haki zake. Amesema, utawala huo ndicho chanzo cha migogoro, mauaji, na ugaidi wa kitaasisi katika eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima kwa ujumla.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, ana matumaini tawala za nchi za Kiislamu zitazingatia vilivyo mateso wanayoendelea kupata Wapalestina na kuchukua hatua ambazo zitatumikia mustakbali mzuri wa taifa hilo madhlumu.

Post a Comment

 
Top