Kenya sasa inataka
faili za kesi zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia
ushahidi wa mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo.
Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.
Ameongezea kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika mahakama hiyo utaangaziwa na Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa haijaanza harakati za kujiondoa.


Post a Comment