Reinhard Grindel amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la Kandanda la
Ujerumani – DFB, na kupewa jukumu la kurejesha uaminifu kufuatia kashfa
iliyotokana na malipo ya kutatanisha kabla ya Kombe la Dunia la 2006
Shirikisho hilo la kandanda lenye ushawishi mkubwa lilitikisika kabisa kutokana na kashfa hiyo iliyozunguka dimba la Kombe la Dunia la mwaka wa 2006 nchini Ujerumani.
Uchunguzi wa kampuni moja ya sheria haukupata ushahidi wa kununuliwa kura kabla ya dimba hilo, ijapokuwa haikufutilia mbali suala hilo. Ripoti hiyo iligundua kuwa DFB iliipa Qatar zaidi ya dola milioni 10 malipo ambayo hayakueleweka. Franz Beckenbauer na maafisa wengine wakuu wa Kombe la Dunia la 2006 wanafanyiwa uchunguzi na kamati ya maadili ya FIFA.
Post a Comment