Ongezeko la idadi
ya watu wanaonyongwa ulimwenguni lilisababisha watu zaidi kuuawa kwa
njia hiyo mwaka uliopita ikilinganishwa na kipindi chochote tangu mwaka
1989,shirika la haki za kibibaadamu la Amnesty International limesema.
Iran,Pakistan na Saudia Arabia walihusika na asilimia 89 ya watu wote walionyongwa duniani.
Jumla hiyo haishirikishi China ambapo Amnesty International imesema kuwa maelfu zaidi waliuawa lakini rekodi zake zikafichwa.
Kwa upande mwengine,kundi hilo limesema kuwa kwa mara ya kwanza mataifa mengi duniani yalifutilia mbali hukumu ya kunyonga.
Mataifa ya Fiji,Madagascar ,Congo Brazaville na Suriname yalibadilisha sheria zao mwaka 2015,huku Mongolia ikipitisha sheria mpya itakayoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu.
Amnesty imesema kuwa China bado inaongoza miongoni mwa mataifa yanayonyonga watu.Inakadiriwa kwamba maelfu ya watu walinyongwa huku maelfu ya wengine wakipewa hukumu ya kunyongwa mwaka 2015.
Post a Comment