Uuzaji wa mafuta ya
Iran umefikia kiwango kikubwa zaidi cha mapipa milioni mbili kwa siku
kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa vikwazo vya kiuchumi mapema mwezi
Januari.
Wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema Iran,
itaendelea kuongeza kiwango cha uzalishaji na uuzaji wa mafuta yake nchi
za nje hadi itakaporejelea kiwango chake cha mapipa milioni 2 na laki
tano ilichokuwa ikiuza ng'ambo kabla ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
Habari hiyo hata hivyo haisaidii mataifa wauzaji wa
mafuta ambao kwa sasa wanateswa na bei iliyoporomoka ya mafuta katika
soko la dunia.
Bei ya mafuta imekuwa ikiporomoka kwa takriban mwaka mmoja sasa kufuatia uzalishaji mkubwa uliofanya bidhaa hiyo kukosa soko.
Post a Comment