Na Saleh Ally
ULISIKIA
namna ambavyo karibu kila kona ya dunia walivyokuwa wakiamini Real
Madrid inakwenda kwenye Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona kuchota aibu
katika mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ msimu huu.
Si
Ulaya tu, Tanzania na Afrika kote, wengi waliamini lazima Madrid
ingefungwa katika mechi hiyo ya juzi usiku kwa kuwa Barcelona
inayoongoza La Liga ina kikosi bora kabisa, tena watendaji kazi ya
ufungaji watatu sasa ni kama ndugu na hawakamatiki.
Lionel
Messi, Luis Suarez na Messi walipachikwa jina la MSN walionekana
watafanya yao na hakuwa wa kuwazuia huku wale wapinzani wao Karim
Benzema, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo maarufu kama BBC wakionekana
kuwa wamedoda kwani hata timu yao iko katika nafasi ya tatu na ilikuwa
na tofauti ya pointi 10 dhidi ya Barcelona.
Safari
ya Camp Nou, kwa maana ya mtazamo haikuwa inaonekana ni nzuri kwa
Madrid. Lakini wengi wakiwemo wachambuzi hawakuwa na subira kuona kocha
mpya wa Real Madrid ambaye alikuwa anaiongoza timu yake katika El
Clasico ya kwanza akiwa mwalimu, atafanya nini.
Kocha
huyo amefanikiwa kuiongoza Madrid kuitwanga Barcelona kwa mabao 2-1,
mabao ya Karim Benzema na Cristiano Ronaldo na bado ikaonyesha soka safi
la kitabuni.
Zinedine
Yazid Zidane si mgeni wa El Clasico, amecheza tokea enzi za Kocha wa
Barcelona, Luis Enrique lakini hata mshambuliaji nyota wa Barcelona,
Messi pia amepambana naye.
Kwa
Zidane, El Clasico ni kitu anachokijua kwa undani. Anaujua ukali na
ubora wa Barcelona kwa vitendo kwa kuwa amecheza. Si rahisi
kumlinganisha na Rafa Benitez au Carlo Ancelotti hata kama wao ni
makocha wakubwa.
Kuijua
El Clasico, haina maana Zidane hatofungwa lakini kwa kuwa ni El Clasico
yake ya kwanza, lazima ilikuwa afanye kitu tofauti, hicho ndicho
kilichoimaliza Barcelona juzi usiku.
Kwa
namna Madrid ilivyocheza, hesabu ya kwanza ilikuwa ni kuwaweka mfukoni
MSN ambao utaona walikuwa ‘likizo’, utafikiri hawapo. Walijaribu lakini
mtego wa Zidane ukawamaliza.
Mbili
ilikuwa kuziba mianya ya mipira inayopitishwa katikati ya uwanja, kama
ambavyo wamekuwa wakifanya Barcelona wakimtumia Messi au Iniesta. Tatu
ni kupokonya mipira kwa haraka na kushambulia kwa mtindo wa kuvuruga.
Lakini
mwisho, utaona mwanzo hadi mwisho wa mchezo, wachezaji wanne
hawakuondoka kabisa nyuma ya mpira. Unaweza kusema Madrid walipaki
angalau basi dogo aina ya Hiace lakini kila waliposhambuliwa, likawa
basi kubwa kabisa kama Ngorika kwa kuwa wote walirejea na kuacha watu
wawili tu mbele.
Uchezaji
wa Barcelona na Madrid kimfumo umekuwa ni 4-3-3. Lakini Zidane
akarejea kwenye mfumo mama wa 4-4-2 ambao ulionekana kuwazima kabisa
Barcelona.
Chanzo
cha kwanza cha uzimaji wa jaribio la MSN ilikuwa ni kumtumia kiungo
mkabaji Carlos Casimiro maarufu kama Casemiro ambaye hata katika
upangaji wa timu kabla ya mchezo ni 9% ndiyo walitabiri huenda
angecheza, lakini akawa chaguo la kwanza la Zidane.
![]() |
CASMIRO VS SUAREZ |
Lakini
unaona Zidane anawachanganya zaidi Barcelona kwa kuwa anawatumia viungo
wote ambao hucheza, yaani Luca Modric na Toni Kroos. Maana yake
Casemiro anakuwa kiungo wa tatu.
Utaona
safu ya kiungo ya Madrid ilikuwa bora katika ukabaji kwa kuwa kwa
wakati mmoja, Casemiro na Kroos walishuka chini na Modric aliyekuwa
namba saba akaingia kati kucheza kama namba nane. Hivyo katikati hasa
Madrid inaposhambuliwa, palikuwa pamejaa na hapakuruhusu mipango ya
upenyezaji mipira.
Kweli
utaona mara kadhaa, Madrid walikosea, lakini si zaidi ya asilimia 20.
Ndiyo maana hata baada ya nahodha wa Madrid, Ramos alipolambwa kadi
nyekundu, Madrid hawakuwa na haraka ya kufanya mabadiliko kwa kuwa
ilikuwa katika mpango sahihi wa ulinzi.
Lakini
mfumo wa ushambulizi pia, wakati Madrid inatoka nyuma kwenda mbele,
kwanza ilikuwa ni mchezaji mmoja au wawili kukimbia na mpira kwa kasi
kama ambavyo Neymar na Messi hufanya. Utaona bao la kwanza namna Modric
alivyokimbia na mpira, akampa Marcelo naye akafanya sawa, naye kabla ya
kumpa Kroos tayari alibadilishana na Modric na kuingia namba saba
aliyepiga krosi safi kwa Benzema.
Madrid
wangeweza kufunga mabao mengi zaidi kama wangekuwa makini. Barcelona
hawakuwa na mpango B wa maana kwa kuwa walilazimika kutoka katika mchezo
wa mipango ya uhakika na kulazimisha bao la kona kwa kuwa Pepe alifanya
uzembe, Gerard Pique akamtoroka.
Wakati
Barcelona wakiwa nyumbani wanaonekana ni wakali sana, mpango mpya wa
Zidane unaonekana kumvuruga hata Kocha wa Barcelona, Enrique ambaye
haraka hakuwa amejiandaa kuuvunja, ndiyo maana Madrid ikiwa ugenini
ikacheza vizuri zaidi na kufunga mabao mazuri likiwemo lile
lililokataliwa alilofunga Bale ambalo halikuwa na tatizo kama mwamuzi
angekuwa makini.
Kitu
kidogo sana kinaweza kubadilisha jambo katika mechi moja kubwa. Licha
ya kutokuwa na uzoefu kama kocha mkubwa, Zidane ametumia uzoefu wake wa
kucheza La Liga na El Clasico, kuishangaza Barcelona.
Post a Comment