Baada
ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), kocha mkuu
wa timu ya Mwadui ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametamka kuwa
lengo lake kubwa ni kuona kikosi hicho kinatwaa ubingwa wa kombe hilo na
kwenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Mwadui
imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuiondosha Geita Gold
inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Seleman Matola, ambapo sasa
wanasubiri kuchuana na Yanga, Azam au Coastal Union au Simba.
Julio
alisema kuwa sababu kubwa ya kulipigia hesabu kombe hilo la shirikisho
ni kiu yake ya kuona kikosi hicho kinapata nafasi ya kuiwakilisha
Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.
“Sisi
hatuogopi timu yoyote ile ambayo tutapangiwa kwenye mashindano haya
maana malengo yetu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa kombe hili na tuna
kila sababu ya kufanya hivyo kutokana na uimara wa kikosi changu
ambacho kinaweza kucheza na Yanga au Azam na tukawafunga.
”Tunalitolea macho kombe hilo kutokana na kutaka kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa,” alisema Julio.
Post a Comment