Kwa jinsi Magufuli anavyotumbua baadhi ya majipu, kunamuabisha sana mtangulizi wake, Jakaya Kikwete kumfanya Kikwete kuonekana kuwa alikuwa ni rais dhaifu sana, kiasi cha kulea madudu kibao, as if awamu ya JK kulikuwa hakuna lolote la maana lililokuwa likifanyika zaidi ya kulea uzembe, as if serikali ya JK ilikuwa ni serikali goi goi, kazi yake ilikuwa ni kulala tuu usingizi, lakini sasa awamu hii ya Magufuli, "hapa kazi", ndio serikali sasa inafanya kazi!.
Just imagine kama wewe ndio JK, unaposafiri unakutana na ma diasfora wa Tanzania kwenye nafasi nzuri ughaibuni, huku wanalipwa vizuri, unawaomba warudi nyumbani kuja kuutumia ujuzi wao kuijenga nchi, baadhi ya wana diaphora hawa wanaguswa na uzalendo, wanakubali kurudi nyumbani na kuukubali umasikini wetu, lakini wanakuwa wakweli kuwa mishahara ya seikali ni midogo mno kuwavutia kurejea nyumbani, JK unawabembeleza na kuwaahidi utajitahidi kuwaongezea kidogo katika kugawana umasikini, japo hautawalipa kama wanavyolipwa huko ughaibuni, lakini utaboresha boresha zaidi angalau kufikia kiwango cha kumfanya asurvive comfortably, hivyo baadhi yao wanakubali wanarejea nyumbani.
Kwa vile wamekuja kwa promise, wanaamua kutopokea any less than the promised amount, wewe unamuahidhi kufuata taratibu za kufikia kiwango kilichoahidiwa, sasa hata kabla muafaka haujafikiwa, mtu aliyekufuatia uliyemkabidhi kijiti kwa upendo wote, kazi yake ya kwanza ni kuwakomoa baadhi ya wateule hawa!, Magufuli alianza na Bade pale TRA, wakafutia wengine, na jana ndio ilikuwa zamu ya Juliet wa TIC, jee ungekuwa ni wewe JK, utajisikiaje?!.
Anachokifanya Magufuli, is it fair kwa JK, kuwatimua watu wake kwa kuwakomoa, jee anawakomoa hao anaowatumbua, au anamkomoa JK na kumuaibisha kuwa JK alikuwa dhaifu mno, hadi kushindwa kuyatumbua hayo anayoyaita majipu?!.
Jee kuna uwezekano kuna baadhi ambao hawakumchagua Magufuli, (walimchagua yule 'jamaa yetu') lakini sasa wanamfurahia Magufuli kutokana na huu utumbuaji wa majipu, lakini kuna waliomchagua Magufuli, akiwemo Kikwete na wote waliotumbuliwa, ambao kutokana na nyadhifa zao, lazima walimchagua Magufuli, lakini sasa wanajuta?!.
Hii tumbua tumbua ya majipu, imekuwa popular hadi kubadili majina ya watu, wale wote waliotumbuliwa, hawatajwi tena kwa majina yao, bali sasa wanaitwa "jipu", hata majirani zao wanawaona kama ni majibu!, mtu unajitolea kuacha maslahi bora ughaibuni kwa kusukumwa na uzalendo, na kuamua kurejea nyumbani, kuitumikia nchi yako kwa moyo wa kujitolea tuu, mara ghafla unatumbuliwa!, hata jina unabadilishwa unaitwa "jipu", is this fair kweli?!.
Kama JK bado anajisikia proud kumkabidhi nchi Magufuli, kwa haya anayoyafanya na kwa stahili hii, ikiwemo uonevu na kuaibishana, then JK ndio mwenye matatizo!.
Post a Comment