Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema anashangazwa
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya waziwazi upendeleo kwa
Yanga, likionyesha wazi limepania kuisaidia kuwa bingwa.
Akizungumza
katika mahojiano maalum na Salehjembe, Hans Poppe amesema mechi ya
Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 6, imesogezwa hadi
Aprili 16, jambo ambalo ni ujanja kwa kuwa itaahirishwa tena ili Yanga
iendelee kuwa na viporo.
Hans Poppe amefafanua hivi:
Salehjembe: Imesogezwa hadi Aprili 16, sasa hofu yako ni ipi na unajua Yanga ina majukumu ya kimataifa?
Hans Poppe: Kama
Yanga wameshindwa kucheza Aprili 6, swali la kwanza jiulize, mbona Azam
FC watacheza dhidi ya Ndanda. Lakini Kupelekwa Aprili 16 ni danganya
toto.
Salehjembe: Danganya toto kivipi Hans Poppe?
Hans Poppe:
Yanga watakuwa na mechi ya marudiano na Al Ahly kati ya Aprili 19 na
20. Katika hali ya kawaida, watakuwa wanaondoka kati ya Aprili 15 au 16
kwenda Misri. Hauwezi kuniambia watacheza.
Salehjembe: Lakini hilo hauna uhakika?
Hans Poppe: Uhakika
unakuja hivi, Aprili 16 hadi 19 ni siku tatu. Lakini Aprili 6 hadi
Aprili 9 ni hivyohivyo. Sasa kama siku ziko sawa, kwa nini hawakucheza
mechi ya Mtibwa Aprili 9?
Salehjembe: Fafanua kidogo msomaji akuelewe, tafadhari..
Hans Poppe:
Utaona Yanga wameacha kucheza katika kipindi cha tofauti ya siku tatu
hadi wanapokutana na Al Ahly, mechi imesogezwa mbele. Sasa Aprili 19 au
20 watakuwa na mechi ya ugenini inayojumlisha wao kusafiri, unafikiri
watacheza vipi? Kwa nini wasingecheza mechi hii ya nyumbani ambayo
haijumuishi safari?
Salehjembe: Kwa hiyo unafikiri kipi kitatokea?
Hans Poppe:
Ndiyo maana nimesema, hata hiyo mechi imepangiwa siku ambayo itasogezwa
tena kwa kisingizio kilekile ili Yanga iendelee kuwa na mechi za viporo
mbele.
Salehjembe: Lakini kwa nini unaonekana kuwa na hofu na viporo wakati Simba inakusanya pointi zake kwa uhakika?
Hans Poppe:
Kiporo mwishoni kwa timu zinazochuana kileleni ni hatari, hii ni rahisi
sana watu kuingia kwenye ushawishi wa upangaji matokeo.
Vizuri
timu zingemaliza mechi zao kwa pamoja na kufanya mambo yawe “fea”.
Lakini si wengine kutengeneza mazingira ambayo yanaonyesha TFF tayari
wana bingwa wao.
Hii
si haki, hii si sawasawa na hili jambo linaonyesha kiasi gani hakuna
haki katika mpira wa Tanzania. Nimekuwa nikisema sana lakini naonekana
kama mkorofi, lakini sasa mambo yanakwenda hadharani na kila kitu
kinaonekana bila hata tabu au kulazimika kupiga hesabu kwamba TFF
imejipanga kupata bingwa wake.
Post a Comment