Bondia Nick Blackwell raia wa Uingereza amezinduka baada ya kuzimia kufuatiwa kupigwa katika pambano lake dhidi ya bondia Chris Eubank wiki iliyopita.#

Blackwell wenye umri wa miaka 25 alipelekwa hospital baada ya pambano lake kusimamishwa katika raundi ya kumi.

Promota wa kampuni ya michezo ya Hennessey alisema "Bondia huyu alianza kuzungumza na familia yake na rafiki zake siku ya jumapili.

Bondia huyu alikua alipata matatizo ya kuvuja kwa damu katika fuvu la kichwa na sio ubongo kama ilivyo ripotiwa awali.