0

UEFA CHAMPIONZ LIGI – ROBO FAINALI: LEO BARCA-

UCL-SIT-SAFIUEFCHAMPIONZ LIGI Jumanne na Juamatano inaingia hatua yake ya Robo Fainali kwa Mechi za kwanza.
Jumanne zipo Mechi 2 ambapo Mabingwa Watetezi FC Barcelona wako kwao Nou Camp kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid na nyingine ni huko Munich, Germany wakati Bayern Munich watacheza na Benfica ya Portugal.
Jumatano pia zipo Mechi 2 ambapo Paris St-Germain wapo kwao Jijini Paris Nchini France kucheza na Manchester City ya England na nyingine ni huko Germany kati ya Wolfsburg na Real Madrid.
Marudiano ya Robo Fainali
PATA DONDOO FUPI ZA MECHI HIZO:
Jumanne Aprili 5
BARCELONA v ATLÉTICO MADRID
-Barcelona wameshinda Mechi 6 zilizopita dhidi ya Atletico Madrid lakini katika Mechi yao pekee ya Ulaya, Atletico iliibwaga Barca kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi 2 za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2013/14.
-Luis Suárez, Neymar na Lionel Messiwameifungia Barca Bao 42 kati ya 51za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.
BAYERN MUNICH v BENFICA
-Bayern imeitupa nje Benfica mara zote 3 walizokutana kwenye Mechi za Ulaya ambazo ni Kombe la Ulaya, Mwaka 1975/76 na 1981/82, na UEFA CUP 1995/96.
-Robert Lewandowski ameifungia Bao 10 Bayern katika Mechi 7 zilizopita za UEFA CHAMPIONZ LIGI Uwanjani kwao Allianz Arena.
-Nicolas Gaitan ndie mpishi wa Bao zote 3 za Benfica kwenye Raundi iliyopita ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.
Jumatano Aprili 6
PARIS SAINT-GERMAIN v MANCHESTER CITY
-Timu hizi zimekutana mara 1 tu Ulaya, Desemba 2008, kwenye UEFA CUP Uwanjani Etihad na Mechi kwisha 0-0.
-Zlatan Ibrahimovic amepachika Bao katika Mechi zote 4 zilizopita za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-Sergio Aguero amefunga Bao 16 katika Mechi 18 alizoanza za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
WOLFSBURG v REAL MADRID
-Wolfsburg hawajawahi kukutana na Real.
-Real ni moja ya Klabu 2 ambazo hazijafungwa kwenye Mechi za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu, huu nyingine ikiwa ni Mabingwa Watetezi Barcelona.
-Real hawajafungwa hata Bao 1 katika Mechi zao 7 kati ya 8 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.
-Cristiano Ronaldo wa Real ndie aliefunga Bao nyingi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI kupita Mchezaji yeyote, Bao 90, huku Msimu huu akiongoza akiwa na Bao 13.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Aprili 5
Bayern Munich v Benfica
Barcelona v Atletico Madrid
Jumatano Aprili 6
Paris St-Germain v Manchester City
Wolfsburg v Real Madrid
Marudiano
Jumanne Aprili 12
Manchester City v Paris St-Germain
Real Madrid v Wolfsburg
Jumatano Aprili 13
Benfica v Bayern Munich
Atletico Madrid v Barcelona
UEFA CHAMPIONZ LIGI
TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28

Post a Comment

 
Top