MADRID, HISPANIA
MSHAMBULIAJI
wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale, amedai kwamba katika mchezo wa El
Clasico uliopita dhidi ya Barcelona hakuwa katika ubora wake, lakini
kwenye mchezo huu ujao atawashangaza mashabiki.
Katika
mchezo wa awali, Madrid walikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, Santiago
Bernabeu na kukubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya wapinzani wao,
Barcelona. Jumamosi ya wiki hii Madrid wanawafuata Barcelona kwenye
Uwanja wa Nou Camp, huku wakiwa na lengo la kulipa kisasi.
“Najua
katika mchezo wa awali dhidi ya Barcelona sikuwa kwenye ubora wangu,
lakini kwa sasa nipo vizuri na ninaamini nitawashangaza mashabiki kwa
kile ambacho nitakifanya.
“Tunaujua
ubora wa wapinzani wetu, lakini hakuna wasiwasi kwa kuwa kila kitu
kinawezekana kwa upande wetu, tunaweza kufanya makubwa kwa kuwa kwenye
kikosi kuna wachezaji ambao wana uwezo mkubwa.
“Barcelona
kwa sasa inaongoza Ligi, lakini hata sisi bado tuna nafasi ya kuwa
mabingwa kutokana na michezo iliyobaki na kama wapinzani wetu watapoteza
michezo yao ijayo,” alisema Bale.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 26, aliweka rekodi ya usajili wake mwaka
2013, ambapo alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 85.3 akitokea
Tottenham.
Post a Comment