NEW YORK, MAREKANI
NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Kehlani Parrish, amekimbizwa hospitali baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujiua.
Mrembo
huyo mwenye umri wa miaka 20, alifikia hatua hiyo kutokana na baadhi ya
watu kudai kwamba ni msichana mbaya katika mapenzi.
Inadaiwa
kwamba mrembo huyo ana tabia mbaya kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi
kutokana na kutodumu nao na huwa akiwaacha wakiwa katika mazingira
magumu.
Lakini
hali ya msanii huyo kwa sasa inaendelea vizuri na ameweka ujumbe kupitia
akaunti yake ya Instagram huku akiwa hospitali na kuandika: “Niliamua
kuchukua hatua hii baada ya kusemwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii
kuwa sio mwanamke mzuri.
“Niliona
bora nipoteze maisha yangu kuliko kuishi katika dunia hii ambayo ina
kila aina ya majungu hasa pale ninapokuwa na mwanaume mpya, ila kwa sasa
naendelea vizuri japokuwa nipo hospitalini,” aliandika Kehlani.
Post a Comment