Dk. Shein alimteua Balozi Iddi kushika wadhifa huo, wiki iliyopita kwa mujibu wa kifungu cha 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.
Uteuzi wa Balozi Iddi ni uteuzi wa pili wa kufanywa na Rais Dk. Shein tangu alipoapishwa Alhamisi iliyopita kuanza kipindi chake cha pili.
Sherehe hizo, zilifanyika Ikulu Zanzibar zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu, Said Hassan Said.
Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu Sheikh Omar Kabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi, Abdallah Mwinyi Khamis na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Khatib Abdulrahman Khatib.
Post a Comment