MKAZI wa Uvinza mkoani Kigoma, Idris Sadala (65), amekutwa amefariki dunia kwenye nyumba ya wageni ya wageni ya New Legeza Mwendo iliyoko mtaa wa Kisangani, Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11:40 jioni kwenye nyumba hiyo na kwamba Sadala alikutwa amefariki dunia katika chumba alichokuwa amepanga.
Alisema Sadala alifika kwenye nyumba hiyo Juni 6, mwaka huu na kupanga chumba namba 101 na siku iliyofuata saa 12 jioni, aliingia chumbani kulala na hakuamka tena.
Kamanda Mtui alisema juzi baada ya baada ya kuona ukimya umetawala katika chumba chake, wahudumu wa nyumba hiyo walienda kutoa taarika katika kituo kikuu cha polisi kwa kutoonekana kwa mteja wao kwa muda wa siku mbili tangu alipoingia kulala.
Kutokana na taarifa hizo, mtui alisema polisi walifika eneo la tukio na kufungua mlango wa chumba na kukuta mgeni huyo akiwa amefariki dunia.
Alisema ndani ya chumba hicho, polisi walikuta chupa moja ya soda aina ya Coca Cola ikiwa imebaki kidogo na chupa ya maji pamoja na vibahasha vinne vya dawa mbalimbali za hospitali ambazo bado hazijatambuliwa na watalaamu wa afya.
Kutokana na hali hiyo, alisema polisi walichukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa Maweni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi pamoja na kutambuliwa na ndugu.
Pia alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na uchunguzi wa kifo hicho unaendelea.
Kamanda Mtui aliwataka wamiliki wote wa nyumba za wageni kuchukua taarifa muhimu za wateja wao pindi wanapowasili zikiwomo jina, kazi, mahali anakoishi, anakotoka na anakokwenda.
Kwa kufanya hivyo, Mtui alisema itakuwa rahisi pindi wateja hao wana[pokumbwa na matatizo ikiwamo vifo.
Post a Comment