0


Bondia raia wa England Anthony Joshua usiku wa April 29 2017 aliingia ulingoni katika uwanja wa Wembley kupambana na bondia Wladimir Klitschko wa Ukraine katika pambano la uzito wa juu.

Anthony Joshua ambaye alikuwa katika ardhi ya kwao England katika jiji la London, hakutaka kuwaangusha mashabiki wake waliyojitokeza katika uwanja huo kutazama pambano hilo dhidi ya Wladimir Klitschko ambaye pia ni mzoefu katika mchezo wa ngumi.

Pambano hilo ambalo Joshua mwenye umri wa miaka 27 ambapo alimpiga kwa KO round ya 11 kati ya 12 Wladimir Klitschko mwenye umri wa miaka 41, limemfanya kuwa Bingwa wa dunia wa boxer wa uzito wa juu. 

Post a Comment

 
Top