Headlines za dawa za kulevya bado zimeendelea katika maeneo mbalimbali
nchini ambapo leo March 1 2017 Kamanda wa polisi Dodoma Lazaro Mambosasa
amezungumza na waandishi wa habari na kutoa takwimu ya watuhumiwa
waliokamatwa na kufikishwa mahakamani hadi sasa.
Mambosasa amesema:
Full stori ya Kamanda Lazaro Mambosasa na alivyoyataja majina ya watuhumiwa nimekuwekea kwenye hii video hapa chini…
Mambosasa amesema:
’Katika operesheni ya kipindi cha miezi minne tangu October 2016 hadi January 2017 tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 88 kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kama vile uuzaji, usafirishaji, usambazaji na ulimaji wa dawa hizo‘ –Lazaro Mambosasa
‘Aina ya dawa tulizofanikiwa kuzikamata ni pamoja na heroine, bangi na mirungi na tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea huku wengine utaratibu ili kuwafikisha mahakamani‘ –Lazaro Mambosasa
‘Nawatahadharisha watu wote wenye nia ya kufanya uhalifu au kuja kufanya biashara haramu ya dawa za kulevya katika mkoa wa Dodoma waache mara moja kwani vita hii ni endelevu hakuna mhalifu atakayebaki salama kama akibainika‘ –Lazaro Mambosasa
Full stori ya Kamanda Lazaro Mambosasa na alivyoyataja majina ya watuhumiwa nimekuwekea kwenye hii video hapa chini…
Post a Comment