Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 02 Machi, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya
Pwani, Lindi na Mtwara.
Katika
ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo
na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Leo
asubuhi Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la kiwanda cha
kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd.
kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani na baadaye ataelekea Mkoani Lindi.
Kesho
tarehe 03 Machi, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake
Mkoani Lindi na keshokutwa tarehe 04 Machi, 2017 atafanya ziara yake
Mkoani Mtwara.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Machi, 2017
Post a Comment