0
Hii imetokea March 14 kwenye shule ya kati iliyopo ROCKDALE nchini Marekani baada ya wimbo wa wasanii wanaounda kundi la MIGOS kufanyiwa mabadiliko na mwalimu DAVID YANCEY baada ya kuuimba wimbo huo wa ‘Bad And Boujee’ na kuuita ‘Bad And Losing.’

Aliimba ‘Bad And Losing’ akimaanisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya ABRAHAM LINCOLIN na wafuasi wake juu ya mipango aliyoiweka kitambo hicho. Madhumuni makubwa ni kurahisisha uelewa kwa wanafunzi wake. Alichokifanya mwalimu huyu kimekuwa gumzo mtandaoni huku video hiyo ikisambaa kwa kasi zaidi. Mwalimu huyo alinukuliwa akiimba: Emancipation proclamation, wakati wanafunzi wakicheza kwa kumzunguka huku wakiimba ‘Listen Up, heal the Nation.’

Yancey amesema ametumia masaa manne katika maandalizi ya wimbo huo alioubadilisha na kuweza kutumia katika kufundishia somo la historia darasani. Sio mara ya kwanza kwa mwalimu huyu kufanya hivyo kwani alishabadilisha wimbo wa Adele “Hello” na kuimba “Hello From The Cherokee” na wimbo wa DRAKE “One Dance” na kuuimba “Georgia Geography” mwingine ni “Back To Back” alioubadilisha na kuuimba “Back To Creek” ambayo hii ilihusu kettle creek.

Muziki wa rap maarufu kama HIPHOP umekuwa ni aina ya muziki ambao ni kama zana kwa walimu wengi katika kufundishia kwani hivi karibuni BIG SEAN,ICE CUBE,TY DOLLA SIGN,na MIGOS walimsaidia mwalimu mmoja hivi wa North Carolina anayeitwa MICHAEL BONNER kuubadilisha wimbo wa O.T GENASIS “Push It” kuupeleka kwenye fasihi ndani ya shule yake.

Post a Comment

 
Top