Mtu mwengine
aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri
wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za
taifa kuhusu mgongano wa maslahi.
Philip Bilden ameeleza wasiwasi
wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika
kujitenganisha na biashara zake. Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.
Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.
Post a Comment