Mama Theresa May (59) wa chamacha Wahafidhina (Conservative Party) leo ameteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wa pili mwanamke (baada ya Margaret Thatcher aliyeongoza kati ya mwaka 1979 hadi 1990 na Waziri mkuu wa 12 tokea utawala wa Malkia Elizabeth, na Waziri Mkuu wa 76 wa Uingereza) katika hafla ya faragha iliyofanyika katika kasri ya Malkia Elizabeth jijini London. Na tayari Malkia amemwomba aunde serikali, kuirithi ya Waziri Mkuu wa zamani David Cameron aliyeachia ngazi baada ya kura ya maoni iliyowafanya Waingereza wajitoe Umoja wa nchi za Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment