Untold story! Skendo ambayo haijawahi kuandikwa wala kusimuliwa popote
inayomhusu mwigizaji ‘hot’ wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya
‘Mama Krish’ ni juu ya madai ya kubakwa na mfanyabiashara maarufu wa
Kihindi jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa), alipokuwa na umri wa
miaka 18 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 28, Ijumaa limefukunyua na
kuinyaka.
Chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Uwoya kilichoomba
hifadhi ya jina gazetini kilidai kuwa, tukio hilo limekuwa likimtesa
Uwoya kwenye maisha yake kiasi kwamba kila akilikumbuka huwa anakosa
amani.
KISIKIE CHANZO
“Irene (Uwoya) ana kitu ambacho kinamtesa sana na mara kadhaa amekuwa
akiniambia kuwa, ipo siku atakitengenezea filamu, anazungukazunguka sana
ila alimdokeza mtu kuwa aliwahi kunusurika kubakwa, labda mkijaribu
kumdodosa anaweza kuwapa ukweli,” kilifunguka chanzo hicho na kuongeza:
“Chondechonde asijue tu kwamba mimi ndiye nimewaambia maana alisema
skendo hiyo ikiandikwa magazetini na dunia ikajua kilichompata, anaweza
akajifungia ndani mwaka mzima kwa aibu.”
UWOYA ANASEMAJE?
Baada ya kuinasa habari hiyo, Ijumaa lilifanya jitihada za makusudi za
kumsaka mlimbwende huyo aliyeshiriki Shindano la Miss Tanzania 2006/07
na kushika nafasi ya tano ambapo baada ya kubanwa ipasavyo kwa kuwa
alikuwa hataki kusikia habari hiyo, alikiri kunusa skendo hiyo ila
akafafanua kuwa, si kweli kwamba alibakwa bali ilibaki ‘kiduchu’ kitendo
hicho kikamilike.
“Nikiri tu kwamba ni tukio ambalo sijawahi kulisimulia popote lakini kwa
kuwa umenibana, ngoja niseme kilichotokea ili iwe fundisho kwa
wengine,” alisema Uwoya na kuendelea:
“Sikumbuki ilikuwa mwaka gani ila ni kweli nilikuwa na kama miaka 18.
Nilikuwa na tabia ya kwenda na wenzangu kwenye nyumba ya mfanyabiashara
mmoja ambaye alikuwa jirani yetu, Mbezi- Beach (naomba nisimtaje)
kuangalia muvi.
“Siku moja, tukiwa kwenye sebule ya tajiri huyo ambaye ana asili ya
Kihindi aliyekuwa akiishi peke yake, aliniita chumbani kwake.
“Kwa kuwa tulikuwa tumezoeana sana, sikuwa na wasiwasi wala kudhani
angeweza kunifanyia jambo baya. Hee! Ile kuingia ndani si akafunga
mlango, wenzangu kule sebuleni hawakujua chochote. Alichokifanya ni
kunilazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu, akaanza kunivua nguo,
nikaona hapa nimekwisha.
“Nilichokifanya nilipiga kelele huku nikipiga ule mlango ndipo wale
wenzangu walipokuja na kutaka mlango ufunguliwe, jamaa alipoona kimenuka
alifungua mlango akatoka nduki na kutokomea nje.”
TAARIFA YAFIKA KWA WAZAZI
Kufuatia tukio hilo, Uwoya alifikisha taarifa kwa wazazi wake ambapo
baba yake, Mzee Pancras Uwoya alilivalia njuga na kumfungulia kesi
mfanyabiashara huyo, kesi ambayo ilinguruma kwa muda mrefu.
“Ni tukio ambalo liliwashangaza wengi na sikumbuki hasa kilichoendelea
ila ninachojua yule mfanyabiashara alitoa fedha nyingi kwa kitendo kile
cha kunidhalilisha,” alifunguka Uwoya.
ANAFICHA KUBAKWA?
Alipobanwa juu ya madai kuwa alibakwa ila hataki watu wajue kuwa
alifanyiwa kitendo hicho, Uwoya alisema: “Kwa kweli hakufanikisha azma
yake, alilazimisha kunivua nguo kweli lakini hakufanikiwa baada ya mimi
kupiga kelele.
KWA NINI AMEFUNGUKA LEO?
“Nimeamua kuliweka wazi kwa kuwa umenibana juu ya ishu hiyo na ili watu
wajue kwamba sijawahi kukwaa skendo ya kubakwa ‘pasee’ ila nilinusurika
kubakwa. Lakini pia nimefanya hivi ili kuwapa fundisho wasichana wengine
kutomuamini kila mtu, kwani aliyetaka kunifanyia kitendo hicho ni mtu
ambaye sikumdhania.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment