0


Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia

Post a Comment

 
Top