Anna
Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson
Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Tukio
hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga
mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa
pole kwa familia ya Kabwe.
Wakati
Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza
mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake
wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.
Kitendo
hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili
19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda
alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini
mikataba iliyoikosesha mapato serikali.
Kabwe
alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli
yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam
alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa
kiume na mmoja wa kike.
Post a Comment