Mkazi
wa Kitongoji cha Kapembo, Kijiji cha King’wangoko wilayani Kaliua, Mkoa
wa Tabora, ametiwa mbaroni akituhumiwa kumuua, mama yake mzazi ,
Kiziko Lukambwe kwa kumnyonga kisha kumtundika ndani ya nyumba
waliyokuwa wakiishi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema kijana huyo anatuhumiwa
kumnyonga mama yake na kumning’iniza ndani ya nyumba, ili ichukuliwe
kuwa amejinyonga.
Issa
alieleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha mauaji hayo na
kwamba, polisi wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi.
Alionya wanaofanya uhalifu hawatapata nafasi ya kukimbia mkono wa sheria.
Majirani wa Kiziko, walieleza kwamba mwanamke huyo amekuwa akilalamika kuwa haelewani na mtoto wake.
“Kiziko inaelekea hakuwa na uhusiano mzuri na mwanaye kwa vile alikuwa akilalamika kuwa, hawaelewani,” alisema mkazi wa Kona nne, Yuda Ngati.
Wilaya ya Kaliua ina matukio mengi ya mauaji yatokanayo na sababu mbalimbali, ikiwamo ulipizaji visasi na imani za ushirikina.
Kamanda Issa aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kwamba, Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo.
Post a Comment