Msanii wa Kimataifa kutoka nchini
Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam
na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika
Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika
la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security,
Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group
pamoja na Coca Cola.
Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza
katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba
ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q,
Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince,
Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii
Neyo.
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The
Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka
Festival 2016 ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika
la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security,
Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.
Meneja Masoko wa CFAO Motors
Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha
msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz
GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla
ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show
love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE
350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere
akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Msanii wa kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo
jioni.
Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya
blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda
kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la
Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe
Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew' iliyoambatana na msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya
Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival
2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe
Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka
nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao
ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua
jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini
wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la
Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF
Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na
Coca Cola.
Baadhi ya wapiga vyombo
waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya
shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza jioni. Kampuni
ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka
Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP
Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo
Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (wa pili
kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon wakiwasili na
katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti
kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla,
Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji
wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja.
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto
mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili
jijini Mwanza leo jioni.
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi
kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki
na kumvisha shuka la Kimasai. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania
ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na
Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK
Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM.
Msanii wa kikundi cha ngoma cha
Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza akimshikisha nyoka aina chatu
msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili katika
uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
Wakazi wa jijini Mwanza
wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha waliofika kumlaki
katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Msanii Neyo alipowasili kwenye
hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza akiwapungia wafanyakazi
pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Mwanasheria wa Jembe Media Group,
Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka
nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe
Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa
kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza kesho
katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Post a Comment