Maafisa wa Serikali ya Canada
wamesema kuwa moto mkubwa, hatari na usioeleweka unatazamiwa kuvuka
mpaka wa Mkoa masaa machache yajayo.
Maafisa hao wana hofu kuwa upepo huenda ukachochea moto huo na wakasema kuwa mvua kubwa isipotokea moto huo utateketea kwa miezi kadhaa.
Mwandishi wa habari wa BBC ambaye ametembelea kambi kadhaa za muda ambazo zinakaliwa na walioondolewa makwao anasema kuwa wamepewa magunia ya vyakula, nguo na vifaa vya watoto kuchezea.
Post a Comment