Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na
Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14,
2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.
Taarifa
ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu
za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya
kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa
Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali
ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku
moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8,
2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu
za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo
wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya
Angola kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo
mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC
ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu
za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7,
2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga
dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika
Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho Mei 3, 2016 kwa
mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa
Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano
Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya
Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam.
Post a Comment