0



Ule ushindani mkali kati ya makocha Jose Mourinho na Pep Guardiola sasa unahamia nchini England.

Tayari Guardiola amesaini kuanza kazi Manchester City huku Jose Mourinho akitarajia kutangazwa leo kuanza kuinoa Manchester United.

Wanajulikana namna ushindani wao mkali ulivyoifanya Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga kuwa na msisimko mkubwa.


Uwepo wao kwenye Premier League msimu ujao, kutaamsha msisiko upya ukilinganisha na miaka miwili iliyopita, Premier League imeonekana kuwa “si ile”.

Post a Comment

 
Top