Kuna ripoti kwamba mchakato wa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
kukabidhi nafasi hiyo kwa Rais Magufuli umekuwa ukisuwasuwa kutokana na
madai kuwa mwenyekiti huyo hataki au anachelewsha kwa makusudi.
Jambo hilo linalelezwa kuzusha mgawanyiko ndani ya chama hicho kikongwe
barani Afrika. Kufuatia taarifa hizo DW imezungumza na msemaji wa CCM,
Christopher Ole Sendeka na kwanza ameulizwa yaliyotokana na kikao cha
Kamati Kuu cha Mei 3 mjini Dodoma.
Post a Comment