Waasi nchini Sudan
Kusini wanasema kuwa wanachama wake 16 wa kitengo cha habari,
wamekamatwa na kupigwa vibaya na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa
nchi hiyo Juba.
Kundi hilo la waandishi wa habari lilikuwa
limetanguliwa katika mji mkuu wa Juba, siku kadhaa kabla ya kuwasili
kwa kiongozi wa waasi Dkt Riek Machar.Dkt Riek Machar anatarajiwa kutawazwa kuwa makamu wa rais kulingana na mkataba wa amani uliositisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza Desemba mwaka wa 2014 kati ya waasi wanaomuunga mkono bw Machar na wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir.
Walikuwa wakijaribu kuwakusanya watu ili kumkaribisha naibu mwenyekiti vuguvugu la waasi, Alfred Ladu Gore.
Hapo jana Jumatatu, zaidi ya waasi wapatao 1,300 walisafirishwa kwa ndege hadi Juba, kama ilivyohitajika katika muafaka wa amani uliotiwa saini majuzi.
Walitakiwa kuhakikisha kuwa usalama wa Bwana Machar, ambaye aliteuliwa majuzi kuwa makamu wa Rais, uko sawa
Post a Comment