Shirika la afya
duniani WHO linasema kuwa viwango vya ugonjwa wa kisukari vinaonyesha
kuwa sasa karibu mtu mmoja kati ya kumi na moja wameathirika na maradhi
hayo duniani .
Katika ripoti yake ya kwanza kuhusu ugonjwa wa kisukari , WHO linasema ugonjwa wa kisukari ulisababisha vifo vya watu milioni moja na nusu mwaka 2012, na nchi zinazoendelea zinaendelea kuathirika zaidi .
Kwa mujibu wa data za hivi karibuni , nchi zilizopo magharibi mwa Pasific vilikua na ongezeko kubwa zaidi la vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kisukari.
Huku watu wakizidi kuongeza uzito ambapo kati ya watu watatu mmoja sasa ana uzito wa kupindukia, ndivyo visa vya waathirika kisukari inavyoongezeka.
Kushindwa kudhibiti viwango vya sukari katika damu kuna athari kubwa kiafya.
Inaongeza hatari ya kushikwa na magonjwa ya moyo na inasababisha kwa mara ishirini watu kuishia kukatwa mguu pamoja na kuongeza hatari ya kuugua magonjwa mengine kama mapafu kuacha kufanya kazi, kuishia kuwa kipofu na matatizo ya uja uzito.
Post a Comment