BAADA ya
nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu nchini Marekani, Lamar Odom,
kuendelea na ulevi wa pombe, mpenzi wake, Khloe Kardashian, amedai
uhusiano huo utavunjika kutokana na pombe.
Oktoba
mwaka jana, Odom alikimbizwa hospitali na kulazwa kutokana na matumizi
ya dawa za kulevya pamoja na pombe kupita kiasi, hivyo baada ya kutoka
katika hospitali hiyo madaktari walimshauri aachane na ulevi huo lakini
wiki iliyopita alionekana akirudia ulevi huo.
Khloe amedai anampenda sana Odom, lakini anaamini pombe zitamsababishia kifo mpenzi wake huyo na kuwa mwisho wa uhusiano wao.
“Odom
ananiumiza kichwa, hospitali aliambiwa asinywe pombe lakini ameanza
tena, hii inanipa wakati mgumu nikiamini kwamba kifo chake kitatokana na
pombe, sina mpango wa kuachana naye lakini pombe inaweza kututenganisha
kwa kupoteza maisha,” alieleza Khloe.
Post a Comment