Kamandi ya oparesheni za pamoja za vikosi vya Iraq imetangaza
kuwa mji wa Hit ulioko mkoani Al-Anbar umekombolewa kikamilfu baada ya
mapigano makali ya wiki kadhaa na magaidi wa kundi la ukufurishaji la
Daesh.
Kamandi ya oparesheni za pamoja za vikosi vya Iraq imetoa taarifa na
kutangaza rasmi kuwa vikosi vya pamoja vya kupambana na ugaidi
vimeukomboa kikamilifu mji wa Hit.
Sabah Al-Nouman, msemaji wa shirika la kupambana na ugaidi la Iraq amesema, oparesheni ya kuukomboa mji wa Hit ilikamilika hapo jana na kwamba magaidi wote wa kundi la kitakfiri la Daesh wametokomezwa na kutimuliwa katika mji huo.
Baada ya kuukomboa mji wa Ramadi ambao ni makao makuu ya mkoa wa al-Anbar, mwishoni mwa mwezi uliopita wa Machi, vikosi vya Iraq vilianzisha oparesheni maalumu kwa lengo la kuukomboa mji wa Hit.
Mji wa Hit ulikuwa umetekwa na kushikiliwa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh tangu tarehe 22 Juni mwaka 2014.../

Post a Comment