0


                                    Marehemu Salah Farah akiwa hospitalini
Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.
  •                                                      Rais Kenyatta alihutubia taifa
Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.

Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab.
Rais Kenyatta amemtuza Mwalimu Farah heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu.

Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.

Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi.

Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja.

Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab.

Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu.

Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa

Post a Comment

 
Top