Mshambuliaji wa klabu ya Leeds United Souleymane Doukara, amepigwa marufuku ya mechi nane kwa kumng'ata mchezaji mwingine.
Doukara ambaye alipinga hatua hiyo pia amepigwa faini ya dola 5000.
Leeds United imekasirishwa na matokeo ya kisa hicho pamoja na urefu wa hukumu lakini imesema haitatoa taarifa zaidi kwa sasa.
Marufuku hiyo inamaanisha kuwa hatashirika kandanda hadi wakati mechi ya mwisho ya msimu.
Post a Comment