0



Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa mara ya kwanza amezungumzia utawala wa Rais Dkt John Pombe Magufuli huku akimpongeza utendaji kazi wake unavyokwenda.

Rais Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

Mzee Mkapa aliyesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumzia ni utawala wa Rais Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, masuala ya uchumi.

Alisema Mkapa kuwa, wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa madarakani bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao.

Post a Comment

 
Top