Viongozi
wawili wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja
kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Kiongozi
wa Movement for Democratic, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa makamu wa
rais wa nchi hiyo Joice Mujuru wa National people's Party walitia saini
makubaliano hayo siku ya Jumatano.
Rais
wa nchi hiyo Robert Mugabe awali alitoa maneno ya dhihaka kutokana na
mipango ya upinzani aliyodai kuungana kumuondoa madarakani.
Morgan
Tsvangirai na Joice Mujuru wameonekana kumaliza baadhi ya tofauti
zao.Tsvangirai anasema makubaliano yaliyotiwa saini baina ya vyama
viwili ni msingi kuelekea kuunda umoja wa vyama kwa ajili ya kupambana
na chama tawala Zanu PF.
Changamoto iliyopo hivi sasa ni kuamua nani kati ya hao wawili ataongoza muungano huo.
Tayari, vyama vingi vidogo vya upinzani vimemuidhinisha Morgan Tsvangirai kuwa mgombea wao wa urais.
Kiongozi wa miaka mingi madarakani Robert Mugabe , alieleza kuwa upinzani umejaa watu wasio na kitu vichwani.
Amesema hakosi usingizi kwa kile kinachoitwa umoja wa wapinzani.
Post a Comment