Ujerumani imeiomba Tanzania kuiunga mkono katika harakati zake za
kutafuta nafasi katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa uchaguzi
utakaofanyika mapema mwaka 2018.
Ujumbe wa Ujerumani umewasilishwa Tanzania na mjumbe maalum wa Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel kwa Rais Dkt John Magufuli na balozi Harro
Adt,na kusema nchi yake inaomba nafasi hiyo huku ikiwa na agenda nne
muhimu.
Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo maalum kutoka Ujerumani kwa
Niaba ya Rais Dkt John Magufuli,Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Tanzania Dkt Agustine mahiga amesema wanatambau mchango wa Ujerumani kwa
taifa na afrika kwa Afrika kwa ujumla.
Katika kutafuta nafasi hiyo katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa
nchi tatu zitakuwa zikiwania nafasi moja huku Isarel na Ujerumani
zikipigiwa upatu zaidi.
Post a Comment