0


Tetesi za kifo cha muigizaji maarufu wa Afrika Kusini, Leleti Khumalo maarufu kwa jina la Sarafina si za kweli kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Hivi karibuni kupitia mitandao zilienea taarifa za kifo cha muigizaji huyo aliyewahi kufanya vizuri kwenye filamu ya ‘Sarafina’ amefariki dunia.

Vyombo hivyo vya habari vimeziita habari hizo kuwa ni uongo wa kupindukia. Mtandao wa wasanii nchini Afrika Kusini unaojulikana kama ‘Mzansi’ ulikanusha taarifa hizo za kifo cha Leleti na kusema ni za uongo na umewatoa hofu mashabiki waliopatwa na mshtuko baada ya kupata taarifa hizo.

Msanii huyo alifanikiwa kutembelea Tanzania mapema mwezi Julai mwaka jana kwenye tamasha la ZIFF lililofanyika visiwani Zanzibar na alialikwa kama mgeni rasmi wa tamasha hilo.

Post a Comment

 
Top