0

Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi bado unaendelea na kwa wale wanafunzi ambao hawajahakiki majina ya wapo kwenye hatari ya kufutiwa mikopo.

Amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa wanafunzi wengi ni hewa kwa kuwa kuna chuo kina wanafunzi 130 wanatakiwa kuhakiki lakini mpaka sasa ni nane tu ndio wamehakiki licha ya kutahadharishwa kufutiwa mikopo yao.

Amesema kwa wanafunzi wanaoenda field fedha zao za kujikimu zimesitishwa kwa kuwa jana walifanya uchambuzi kwenye vyuo viwili na kukuta wanafunzi marehemu na waliofukuzwa wameombewa fedha za field

Post a Comment

 
Top