Obama amewahimiza wanafunzi 2,000, weusi kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi
Rais wa Marekani
Barack Obama amewahimiza wanafunzi 2,000, wengi wao weusi kuimarisha
juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi aliosema umebakia nchini humo.
Akizungumza
katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington, Bw Obama alisema hali
ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika imeimarika sana tangu yeye atoke
chuo kikuu mwaka 1983. Obama awaasa weusi Marekani
Lakini alisema kuchaguliwa kwake kwa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika nchini humo hakujasaidia kupunguza ubaguzi wa rangi.
Bwana
Obama alisema vijana hao wanapaswa kujivunia kuwa watu weusi lakini
lazima wahakikishe kuwa wana mipango kambambe ya kuleta mabadiliko.
Post a Comment