Rais
John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi wa
umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.
Rais
amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili
katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.
Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.
Amesema
analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali
lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.
Rais
huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”, amesema Tanzania ni taifa tajiri,
hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya
kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi
wameanza hadi kupelekwa nje.
"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema
Post a Comment