Akizungumza na Bongo5, Gigy amesema maisha aliyopitia yamemfanya awe ni mwanamke asiyependa kufanya mapenzi.
“Mimi nimepoteza ile ari ya kufanya mapenzi au kuwa na mpenzi mmoja au nijiachie na mwanaume kama mtu na mpenzi wake siwezi, sasa hivi natafuta maisha, pesa mbele,” alisema Gigy. “Kama yeye ana wivu na mimi, mimi sina wivu na mwanaume,”
Gigy amesema taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba anajiuza siyo za kweli, kwani yeye ana mwanaume ambaye anamuudumia kila kitu ingawa hawafanyi mapenzi.
“Nina mtu ambaye ananihudumia, ananipa mtaji ya biashara zangu. Pia hata kwenye muziki anawekeza pesa yake. Kwa hiyo waache wanifikie hivyo wanavyofikiria, mimi nafikiria navyojijua, mimi nipo tofauti sana na wanavyozungumza, ukijaribu kukaa na watu wangu wa karibu watakwambia,” alisema Gigy.
Post a Comment