Gari la kielektroniki la Tesla
Kampuni ya magari
ya Tesla imezindua gari lake lililotarajiwa na wengi aina ya Model
3,likiwa ndilo gari lenye bei ya chini ikilinganishwa na magari mengine
ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa Elon Musk,amesema kuwa lengo lake ni kuzalisha magari 500,000 kwa mwaka.
Magari ya kwanza yataanza kuuzwa mwaka 2017,na yataweza kuagizwa kutoka mataifa mengi,ikiwemo UK,Ireland,Brazil,India,China na Newzealand.
Yale ya kawaida yatauzwa kuanzia dola 35,000 na yana kasi ya hadi kilomita 346 kila linapochajiwa.
Magari mengi ni ya S Saloon, ambalo limelipiku gari la kielektroniki la Nissan Loaf na kuwa gari la kielektroniki linalouza sana duniani.



Post a Comment