0


SABO KAZINI...

Kiungo mshambuliaji hatari wa Coastal Union, Yusouf Sabo raia wa Cameroon amesema Coastal Union ina nafasi kubwa ya kubaki Ligi Kuu Bara.

Lakini amesisitiza kuwa viongozi na wachezaji lazima kwa pamoja wafanye kazi ya ziada kuhakikisha wanabaki.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Sabo amesema ana imani kubwa wachezaji wana nia kuu ya kuhakikisha timu inabaki lakini lazima wajitume.

“Nininaamini wachezaji wa Coastal Union wana hamu kubwa kuona tunabaki ligi kuu. Tunapambana sana tena kwa moyo mmoja. 

“Ukiniambia niwashauri, nitawaambia wapigane vilivyo kwa umoja. Mimi nikiwa mmoja wao lazima tushirikiane na kupambana kwa nguvu zaidi ya mechi zilizopita.

“Kwa upande wa viongozi, kama unavyojua mazingira kwa Coastal bado si mazuri sana. Lakini ni vizuri viongozi sasa wakawa karibu zaidi na wachezaji.

“Wasogee, waboreshe mazingira, tuungane zaidi ya zamani na kupambana kwa nguvu zaidi kuibakisha Coastal Union,” alisema Sabo.
Sabo ni kliboko ya vigogo, kwani alianza kuifunga Yanga kwenye Ligi Kuu Bara, akarudia hivyo kwenye Kombe la FA.

Lakini ndiye aliyeifungia Coastal Union mabao yote mawili wakati ikiitoa Simba kwenye Kombe la FA kwa kuitwanga kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top