Rais wa Marekani
Barack Obama anawasili nchini Saudi Arabia hii leo, wakati ambapo kuna
mvutano kati ya Marekani na Saudia kutokana na vita vya Islamic State na
makubaliano ya nuklia na Iran.
Obama atafanya mazungumzo na mfalme wa Saudi Arabia, Salman kabla ya kuhudhuria mkutano wa nchi za ghuba siku ya Alhamisi.Mhariri wa BBC nchini Marekani ambaye anasafiri na Rais Obama, anasema kuwa watu nchini Saudi Arabia wanahisi kuwa Marekania imewapa mgongo hasusan kuhusu Iran.
Huu ndio mwanzo ya ziara ya wiki moja ya Rais Obama ambayo pia itampeleka nchini Uingereza na Ujerumani.
Post a Comment