Maafisa wakuu wa idara ya Afya nchini Liberia wamethibitisha kutokea kwa kisa cha pili cha mgonjwa wa Ebola.
Aidha tangazo hilo limewadia miezi miwili pekee tangu ugonjwa huo hatari kutangazwa kuisha nchini humo.
Mtoto wa mwanamke mmoja aliyefariki kutokana na ugonjwa huo mapema wiki hii anatibiwa kwenye kituo cha uangalizi mjini Monrovia.
Liberia imefunga mipaka yake kwa muda baada ya visa vya Ebola kuripotiwa nchini Guinea.
Shirika la Afya duniani WHO limesema lina aamini visa vilivyoripotiwa hivi sasa vinaweza kudhibitiwa.


Post a Comment