0


 
Mitsubishi imesema kuwa majaribio ya matumizi ya mafuta yalifanywa kwa njia isiyo sahihi.
Kampuni ya kuunda magari ya Japan ya Mitsubishi, imekiri kufanya makosa katika kueleza takwimu za matumizi ya mafuta kwa zaidi ya magari 600,000.

Mauzo ya hisa za kampuni hiyo yalifunga yakiwa yameshuka kwa asilimia 15 kutokana na ripoti kuwa ilikuwa imedanganya.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mitsubishi ilisema kuwa majaribio ya matumizi ya mafuta kwa magari hayo yalikuwa yamefanywa kwa njia ambayo haikuwa sahihi.

Ilisema kuwa magari yaliyopatwa na kosoro hiyo yalikuwa yametengenezwa kwa kampuni ya Nissan.
Hayo yanajiri wiki sita baada ya kampuni ya magari ya Ujerumani ya Volkswagen, kukiri kudangaya katika mitambo ya gesi chafu ya magari yanayotumia mafuta ya diesel.

Post a Comment

 
Top