Mapigano yameongezeka kuzunguka mji wa pili nchini Syria wa Aleppo jana
Alhamis(14.04.2016), wakati mashambulizi yanayosaidiwa na ndege za
kivita za Urusi yakiathiri makubaliano muhimu ya kusitisha mapigano.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura
Hali hiyo hata hivyo inatishia pia duru mpya ya mazungumzo ya amani mjini Geneva.Wapiganaji wa upande wa serikali, waasi na wapiganaji wa jihadi waliendelea na mapambano katika
azma ya kupata udhibiti wa maeneo ya jimbo la Aleppo, hali inayotishia makubaliano ya karibu wiki saba sasa ya kusitisha mapigano ambayo yameshuhudia ghasia zikipungua kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka mitano ya mzozo huo.
Wawakilishi wa upande wa upinzani katika mazungumzo ya amani ya Syria mjini Geneva
Wapiganaji wanaoiunga mkono serikali wakisaidiwa na ndege za kivita za
Urusi wameendelea na mashambulio makali kaskazini kidogo mwa mji mkuu wa
jimbo hilo Aleppo, limesema shirika linaloangalia haki za binadamu
nchini Syria.Hatari ya kuporomosha usitishaji mapigano
Mapigano yalikuwa makubwa zaidi katika eneo la handarat, eneo la milima ambalo liko katika barabara kuu inayoelekea upande wa kaskazini katika maeneo yanayodhibitiwa na upinzani katika mji huo.
Mkuu wa shirika hilo linaloangalia haki za binadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman amesema majeshi ya serikali, yakiungwa mkono na Urusi na ndege za kivita za Syria, yanataka kuzuwia barabara hiyo na kuzingira kabisa maeneo ya vitongoji vya upande wa mashariki.
Wakimbizi wa Syria wakiwa nchini Uturuki
Mwandishi habari wa shirika la habari la AFP katika maeneo
yanayoshikiliwa na upinzani ya mashariki mwa mji wa Aleppo amesema sauti
za makombora zilisikika siku nzima jana, lakini hakuna kombora
lililoangukia katika mji wenyewe hasa.Mashambulizi hayo yamezusha , kile kilichoelezwa kuwa "wasi wasi mkubwa" katika serikali ya Marekani kuhusiana na usitishaji mapigano, ambao umeshuhudia kupungua kwa ghasia baada ya kuanza kufanyakazi Februari 27.
Marekani yaingiwa na wasi wasi
Afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani amesema mashambulizi hayo, yanaweza kabisa kuathiri hatua ya kuacha uhasama, hali ambayo imo katika mbinyo mkubwa katika wiki za hivi karibuni.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini pia ameelezea wasi wasi wake juu ya mashambulizi ya Aleppo na kutoa wito wa kuheshimiwa , kuimarishwa na kupanuliwa kwa makubaliano hayo.
Rais Vladimir Putin wa Urusi muungaji mkono mkubwa wa rais Assad, amesema katika kipindi ambacho hujibu maswali ya wananchi katika televisheni ya Urusi jana kwamba anafuatilia kwa karibu ongezeko la ghasia hivi karibuni.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini
Wawakilishi wa utawala wa rais Bashar al-Assad wanatarajiwa mjini Geneva
leo Ijumaa kwa ajili ya mazungumzo ya amani na mjumbe wa Umoja wa
mataifa nchini Syria Staffan de Mistura, ambaye ameishutumu serikali ya
Syria kwa kuzuwia juhudi za kufikisha msaada wa kukoa maisha kwa Wasyria
wanaouhitaji."Siwezi kukana kwamba kila mmoja amekatishwa tamaa , na wengi kwa kweli wamefadhaika kutokana na kutokuwapo na misafara mipya inayofika , hususan katika maeneo ambayo yametambuliwa kuwa yamezingirwa, na pia yanatambuliwa na nyaraka za kimataifa."
Vikwazo dhidi ya IS
Urusi kwa upande wake imetoa wito jana wa kufungwa kwa mpaka kati ya Syria na Uturuki ili kuzuwia makundi ya itikadi kali ya Dola la Kiislamu na Al Nusra Front kuingiza wapiganaji na silaha kutoka nje.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vitaly Churkin ameuambia mkutano wa baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu kupambana na ugaidi, kwamba wajumbe ni lazima pia wafikirie juu ya kuweka vikwazo kamili vya biashara na kiuchumi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameliambia baraza hilo kwamba zaidi ya watu 30,000 kutoka duniani kote wamejiunga na kampeni ya IS nchini Iraq na Syria.
Post a Comment